MICHEZO

Taarifa Mpya Juu ya Hali ya Mchezaji Thaban Kamusoko

on

Baada ya kushindwa kumaliza mchezo dhidi ya Njombe Mji, kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko amerejea kwenye mazoezi baada ya kupata ruhusa ya daktari.Kamusoko alianza mchezo huo vizuri uliochezwa kwenye Uwanja wa Sabasaba ambapo timu yake ilipata ushindi wa bao 1-0, lakini alishindwa kumaliza dakika 90 ambapo alitoka kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Rafael Daudi hali iliyopelekea kuleta wasi wasi kwa mashabiki wa Timu hiyo yenye maskani mitaa ya Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Haikujulikana kwa haraka juu ya kilichosababisha akashindwa kuendelea kucheza licha ya kutoka uwanjani akitembea mwenyewe bila msaada wa mtu yeyote.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa Kamusoko alipata majeraha madogo lakini alirejea uwanjani Jumatatu na kuendelea na mazoezi kama kawaida baada ya kuruhusiwa na daktari wa timu aliyemfanyia uchunguzi.


IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply