Wasanii

Wolper Aliamsha dude Wimbo Mpya wa Harmonize

on

Septemba 12, 2017. Imekuwa ya kipekee na inaonekana kuwa ya kihistoria katika maisha ya msanii kutoka WCB, Harmonize kwani Baada ya Kuachia wimbo wake wa “Nishachoka” Mapema Leo amekumbana na Kichambo kikali kutoka kwa Mpenzi wake wa Zamani Jackie Wolper.

Wolper ametoa maneno makali kwa zilipendwa wake huyo kutoka Usafini huku akidai kuwa yeye alisha msahau kitambo hivyo msanii huyo aache kumtungia nyimbo za Taarabu. Wolper anahisi wimbo huo wa “Nishachoka” ametungiwa yeye, Ametumia ukurasa wake wa Instagram kwa Kutoa Mapovu Haya:-“Kwahiyo baada ya kuona mm nimeendelea na maisha yangu ukaona unitungie wimbo sumu hahahaha!Uongee ya kurudi asubuhi kisa kwenda kuchukua ela kwa Sarah afu Mm siimbi lkn kuna kitu kinaitwa call recorder nikisema nifanye kitu uenda Sarah atafika Italy kwa mabawa!Unasahau kuwa nina voice zako za juzi kati hapa ulizonipigia unalia lia km king’ora cha wagonjwa wenye hali maututi??Usitake niseme vyote usinichokonoe nimwage mivoice Afu mm sina hasara maana simfich m2 wangu k2. Ila ww na penzi lako la biashara ndo utakaepambana na yule mama kija wako!Niache kidogo bwana imba hata nyimbo ya kuhusiana na Tundu Lissu afu jina unaweka wasiojulikana asee utauza sn kuliko kumuongelea mtu ambae mmeachana afu kaamua ku moooooove on…..!Hivyo yani km umenimiss nipitie hata kwenye kale kanyimbo ulikoniopaka mafuta kwa mgongo wa chupa (#Niambie.) lkn sio kuniendea studio kuniimbia taarabu 🤣🤣Ujue tatizo lako unahisi mwanaume upo ww tu bongo 😝😝Polyeeee sn wimbo nimeusikia lkn nimependa beat tu….!Afu kuongea sipangiwi,kukwepesha ndo kitu niliachaga toka enzi nacheza makidamakida hehehe Kunyamaza kwa vitu vya kijinga pia siwezi hilo ndo tatizo langu….Haya wenye kutoa mapovu toeeeni weeeh nakuja na beseni,pipa km yatalipa ntapeleka dry cleaners niwauzie tupate wateja…!Afu mtakao pata ujumbe pia mscreenshot tu!afu pia sijaongea yotee cz nimejua sikuhizi watu wanauza mziki kwa kuchamba watu,so endelea kufanya kazi yako….!lkn kumbuka na mm msanii nikitoa series ntauza sn cz ni ukweli mtuuuupu 👌” – Hii ni Post ya Kwanza aliyoiandika Wolper.

Hakuishia hapo akaona Bado ndani ya Moyo wake kuna kinyongo zaidi akaamua kuongeza Post Nyingine ambayo nayo ilisomeka kama Ifuatavyo:- Haya kijana post nilizopost zinazo kuhusu zitachukua masaa mawili tu!Maana ukute navyokuweka hata hivi nakupa viewers wa nyimbo yako yenye stress,Na usije ukapata wanaume wenzio wenye stress za wanawake km ww!Tusilazimishane kuongea nimeshaachana na ww kiusalama ongelea vilivyopo sasahivi kwako na sio mm,Nilishatokaga huko kiurahisi unaweza ukadeal na style yako ya mziki bila KUNIHUSISHA maana unampa hofu pia BFF anahisi labda kuna kitu kumbe hakuna,Usiniharibie mahusiano yangu mapya kwa taarabu zako,BFF wangu ni bora kuliko wewe Afu nahisi km hayupo km Huyu yani huyu ni adimu staki kumpoteza kwa ajili ya watu km ww!Km aliweza kuziba maumivu yako na nakuona km trakatraka basi naomba uniache kijana Nimeandika nikijiamini km mtoto wa kike bila kumuogopa mtu yoyote….Nikuahidi usidhani mm Yesu akipigwa shavu la kushoto ageuze na la kulia ili apigwe tena,Mimi ni Jackie Wolper tena Massawe!Ambae siwezi kuacha kuongea ukinianza na maliza!Kwa wale wanaosema bora kunyamaza subirini ya wakute afu ndo mjipe huo ushauri nyie!ASANTENI
#NyamazaKuliaStudio
#NdioUkubwaHuo
#UlipendaPesaKulikoTrueLoveSasaPambanaNaPesaZake
#UmakondePiaAchaUshafikaMjini


IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply