Kitaifa

Rais Magufuli Mgeni Rasmi Kilele cha Mbio za Mwenge na Siku ya Mwalimu Nyerere

on

Rais Magufuli leo Oktoba 12, 2017 amekwea pipa na kwenda visiwani Zanzibar akiwa na mkewe kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo Rais Magufuli anategemewa kuwa Mgeni Rasmi siku ya kilele cha Mwenge wa Uhuru Oktoba 14, 2017 Uwanja wa Amaan.
Rais Magufuli visiwani Zanzibar amepokelewa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kuwasili katika uwanja  wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Grayson Msigwa amesema kuwa Rais Magufuli atakuwepo visiwani Zanzibar kwa siku tatu na kudai pamoja na mambo mengine Rais Magufuli atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na siku ya Mwalimu Nyerere.


IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply