MICHEZO

Taarifa za Usajili wa Simba SC Leo November 12, 2017

on

Klabu ya Simba ipo mbioni kumsajili beki wake wa zamani Miraji Adam kutoka African Lyon, baada ya mchezaji huyo kukiri kuwa katika mazungumzo yao yapo katika hatua za mwisho kabla ya kukamilika na yeye kumwaga wino msimbazi.

Miraji amesema, anahitajika na club yake hiyo ya zamani ili kusaidiana na Ally Shomari ambaye anaonekana kuwa peke yake baada ya Shomari Kapombe kuonekana hatopona hivi karibuni kutokana na ukubwa wa tatizo lake.

“Nikweli mzunguko wa pili naweza kucheza Simba endapo mambo yatakwenda sawa kama tulivyo zungumzo nao lakini kwasasa mimi bado ni mchezaji wa African Lyon, mpaka hapo tutakapomalizana na Simba pamoja na timu yangu ambayo naichezea hivi sasa”.

Mkataba wa Adam na African Lyon, unamalizika mwezi ujao aliweka wazi kuwa yeye hana hiyana kwa sasa kwani timu yoyote itakayomalizana naye ataenda kuitumikia msimu ujao.

“Baada ya Simba kunifuata na kukubaliana wakaniambia watanipigia simu, ila pia Singida United, nao wamenifuata lakini hatujafikia muafaka, nipo nawasikilizia Simba kama wakizidi kukaa kimya na Singida wakieleweka basi nitaachana na ofa ya Simba na kwenda Singida,” alisema Miraji.


IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply