MICHEZO

VIDEO :: John Bocco Aondoa Gundu Sokoine, Simba Ikishinda 1-0 dhidi ya Prisons

on

Leo November 18, 2017. Ligi ya Vodacom iliendelea katika viwanja mbalimbali nchini. Mjini Mbeya Tanzania Prisons iliwakaribisha Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club katika uwanja wa Sokoine.Simba Sc imeibuka mshindi kwa kubeba alama tatu muhimu kwa ushindi wa dakika za mwisho kupitia kwa mshambuliaji wao John Bocco aliyeifunga mnamo dakika ya 84.

John Bocco ameipa Simba ushindi wa kwanza dhidi ya Tanzania Prisons tangu iliposhinda mara ya mwisho 2013 kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.

Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe poini 22 ikiwa inaongoza ligi mbele ya Azam ambayo itacheza kesho dhidi ya Njombe Mji.

NIMEKUWEKEA HAPA VIDEO YA MCHEZO HUO BOFYA PLAY.


IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply