News

Azam Fc yatamba Kuifunga Yanga

Baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Ndanda Fc Mabingwa wa Afrika mashariki Azam fc wamepanga kumaliza hasira zao kwa vinara wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga katika mchezo wao wa kiporo utakaopigwa April 29 mwaka huu katika dimba la uwanja wa Taifa.

Azam Fc yatamba Kuifunga Yanga

Meneja wa Azam Philipo Alando amesema kuwa wamerejea Dar es salaam  tayari kwa maandalizi ya kuwavaa Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu kwani wamedhamiria kupata ushindi licha yakuwa wanawaheshimu Yanga SC.

“Ni mechi ngumu sana ukiangalia wao wamejipanga na sisi tumejipanga sana kuhakikisha tunashinda mechi hiyo ambayo itatoa taswira kwetu katika kuwania nafasi za juu katika msimamo huo” amesema Alando.

Aidha Alando ameweka wazi kuwa wamepokea kwa furaha taarifa za kutoka CAF juu ya Tanzania kuingiza timu nne katika mashindano ya kimataifa huku akizitaka timu zitakazo pata nafasi hiyo zisibweteke .

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker