News

Azam FC Yaungana na Simba Kimataifa

TIMU ya Azam FC imefuzu michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika msimu ujao baada ya kuifunga Lipuli FC bao 1-0 kwenye fainali za Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Azam FC Yaungana na Simba Kimataifa

Mbali na kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika, timu ya Azam imeondoka na kitita cha sh. milioni 50, medani pamoja na kombe.

Fainali hizo zimefanyika Jumamosi, Juni 1, 2019 katika uwanja wa Ilulu, Manispaa ya Lindi ambapo ushindi huo unaifanya Azam FC kuungana na Simba kuliwakirisha Taifa kwenye michezo ya Kimataifa itakayoanza Novemba mwaka huu.

Mshambuliaji wa Azam Obrey Chirwa ndio aliyeiwezesha timu yake ya Azam kuibuka na ushindi katika mchezo huo baada ya kufunga bao la ushindi katika kipindi cha pili.

Azam FC Yaungana na Simba Kimataifa

Katika mchezo huo ulioshuhudiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, timu ya Lipuli FC iliyong’ara kwa kutawala mchezo kwenye kipindi cha kwanza, ilishindwa kutumia nafasi nyingi ilizozipata kuifunga Azam.

Mbali na timu ya Lipuli kuwa mshindi wa pili katika mashindano hayo, pia timu hiyo imetoa mchezaji bora wa mechi ya fainali, Paul Ngalema pamoja na mfungaji bora wa mashindano hayo Seif Rashid na kupata Kitita cha Tsh milioni 25.

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker