Wasanii

Babu Tale Aogopa Kurogwa Kisa Bima za Diamond Tandale

Meneja wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Babu Tale amekanusha madai kuwa msaada wa bima ya afya unaotolewa na msanii wake ni kwa ajili ya watu maalum.Tandale
Tale amelazimika kusema hayo baada ya kuwepo malalamiko ya watu wakiamini kuwa wanaopata waliandaliwa.
Meneja huyo yupo katika uwanja wa Magunia kutoa bima hizo kwa niaba ya Diamond ambaye hadi tunarusha taarifa hii alikuwa bado hajawasili amesema wanatoa bila kuchagua.
“Jamani kutoa riziki ni kazi ngumu ndio maana Mungu amejificha kwahiyo hayo malalamiko yenu nayaelewa hakuna aliyechaguliwa kabla kila kitu kinafanyika hapa hapa, msije mkaniroga bure mie nimetumwa tu. Kijana wenu ameamua kutoa bima hizi kwa ajili ya wanaTandale wote bila ubaguzi ” -Babu Tale
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker