News

Ben Breaker Awashusha Hadhi Mastaa wa Bongo

Wakati wanamitindo wengi wa kiume Tanzania wakijipatia majina makubwa na umaarufu kutokana na kutoka kimapenzi na Wasichana maarufu Tanzania wakiwemo Wasanii wa Filamu Tanzania(Bongo movies).

Ben Breaker Awashusha Hadhi Mastaa wa Bongo

Jambo hilo limekuwa tofauti kwa Mwanamitindo Ben Breaker ambae yeye kajizolea umaarufu kutokana na kazi zake zenye ubunifu ambazo zimepelekea hadi kushinda tuzo za kimataifa.

Mwanamitindo huyo ameeleza kuwa hakuna star wa kike Tanzania anayemvutia kimapenzi, kutokana na mastar hao kutokuwa na uhalisia, ukiwaona kwenye mitandao wako tofauti na jinsi walivyo katika maisha halisi.

Ben Breaker Awashusha Hadhi Mastaa wa Bongo

Ameeleza kuwa wengine kwenye mitandao huonekana na muonekano wa kuvutia lakini ukikutana nao katika maisha ya kawaida wanapoteza mvuto na uzuri ambao unaonekana kwenye mitandao.

Ben Breaker ameeleza hiyo ndio sababu inayomfanya kushindwa kutoka nao kimapenzi ameongeza kusema ni bora atoke kimapenzi na Wasichana wasio na umaarufu kuliko kuwa na mahusiano na wasichana maarufu kutoka Tanzania.

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker