News

CCM Yawasamehe na Kuwarejeshea Uanachama Madabida na Wenzake

CCM Yawasamehe na Kuwarejeshea Uanachama Madabida na Wenzake

Pichani ni wanachama hao waliosamehewa wakiwa wamesimama mbele ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu Mwenyekiti wake Ndg. Philip Mangula na Katibu Mkuu Dkt. Bashiru Ally na mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) wakati wa  Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa leo tarehe Desemba 18, 2018 Jijini Dar es Salaam 

CCM Yawasamehe na Kuwarejeshea Uanachama Madabida na Wenzake

Pichani ni wanachama hao waliosamehewa wakimshukuru Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu Mwenyekiti wake Ndg. Philip Mangula na Katibu Mkuu Dkt. Bashiru Ally  mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) wakati wa  Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa leo tarehe Desemba 18, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuuya CCM Taifa kimefanyika leo tarehe 18 Desemba, 2018 Jijini Dar es Salaam nakuongozwa na Ndg. John Pombe Joseph Magufuli, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kikao hicho kimepokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na taarifa ya chama juu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa CCM ya mwaka 2015.

Pia, kikao hicho kimepokea taarifa kuhusu masuala ya maadili, kimepokea na kuridhia marekebisho ya kanuni mpya za fedha na mali za chama na jumuiya zake na kimepokea na kuridhia uteuzi wa wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa CCM.

Kwa kauli moja Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imepokea maombi na kukubali kusamehewa adhabu ya kufukuzwa uanachama kutoka kwa waliokuwa wana CCM wanne ambao walitenda makosa hayo wakiwa Wenyeviti wa CCM ngazi ya Mikoa na Wilaya.

Waliosamehewa na kurejeshewa uanachama ni;

 1. Ndg. Ramadhani Rashid Madabida (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam).
 2. Ndg. Erasto Izengo Kwirasa (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga).
 3. Ndg. Christopher Mwita Sanya (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara).
 4. Ndg. Salum Kondo Madenge (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni).

Aidha, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwakauli moja imeamua kumuweka katika uangalizi Ndg. Jesca Msambatavangu ambaye ameomba kurejeshewa uanachama wa CCM baada ya kufukuzwa kwa makosa ya kimaadili.

Halikadhalika, Halmashauri Kuu ya CCM imepitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama katika ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa zilizoachwa wazi baada ya waliokuwa katika nafasi hizo kupangiwa majukumu mengine ya Kiserikali au  kufariki dunia pamoja na mgombea wa CCM wakiti cha Ubunge katika Jimbo la Temeke Jijini Dar es Salaam.

Waliopitishwa kugombea nafasi hizo ni kama ifuatavyo.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa

 • Dkt.Damas Mukasa Kashegu
 • Asha Juma Feruzi
 • Galila Ramadhani Wabanhu
 • Makene Pamella Boniphas

Mwenyekitiwa CCM Mkoa wa Iringa

 • Dkt. Abel Mwendawile
 • Aman Said Mwamwindi
 • Sabas Vitus Mushi

Katibu wa Itikadi na Uenezi Mkoa wa Simiyu

 • Mashaka Abeid Makongoro
 • Mayunga Genga Ngokolo
 • Heri Mchunga Zebedayo

Mwenyekitiwa Wazazi Mkoa wa Mwanza

 • BahebeEmmanuel Ezekiel
 • Nyiriza Makongoro Nyiriza
 • Masso Gerald Jane
 • Misogalya Isaac Kilangi Kassile

Mwenyekitiwa Wazazi Mkoa wa Mwanza

 • Salum Mohamed Chima
 • Yusuph Mwandami Gwayaka
 • Bertha Peter Nakomolwa
 • Philemon Josephat Kiemi

Mwenyekitiwa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini

 • Amina Ally Kobo
 • Lemmy Joel Ludovick
 • Hamidi Rajabu Shebuge

Halmashauri Kuu ya CCM imemteua Ndg. Abdallah Ally Mtolea kuwa Mgombea wa kiti cha ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Temeke, Jijini Dar es Salaam.

Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imeiagiza Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) kurudia mchakato wa kupendekeza majina yamgombea wa nafasi ya Mjumbe wa NEC.

Wakati huo huo, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kauli moja imetupilia mbali pingamizi zilizowekwa dhidi ya viongoziwa CCM katika ngazi mbalimbali na kuagiza viongozi hao waendelee na nyadhifa zao.

Pingamizi hizo ziliwekwa dhidi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndg. Anthony Mwandu Diallo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Lindi Ndg. Aisha Ally, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Ndg. Salim Mohamed na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ngara Ndg. George Jackson Rubagora.

Pamoja na kutupilia mbali pingamizihizo, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imewaagiza walezi wa mikoa yote ambayo viongozi wake waliwekewa pingamizi wakutane na wanachama na kukiunganisha chama.

Halmashauri Kuu ya CCM imemuagiza Ndg.Zubeir Majaliwa (aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Uvinza) ambaye Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Uvinza ilimsimamisha uanachama kuwasilisha rufaa yake kuanzia ngazi husika wakati adhabu yake ikiendelea.

Aidha, Halmashauri Kuu ya CCM imetoa adhabu ya KALIPIO kwa mwanachama wa CCM Ndg. Hasnain Murji kutokana kukabiliwa na makosa ya kimaadili.

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker