News

Fatma Karume Aonyesha Mahaba kwa Nay wa Mitego

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Fatma Karume, amefunguka juu ya mapenzi yake juu ya msanii wa muziki wa bongo fleva, Nay wa Mitego.Fatma Karume Aonyesha Mahaba kwa Nay wa MitegoAkipiga stori na Big Chawa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Fatma Karume amesema anampenda sana Nay wa Mitego, kutokana na ubishiwake anaouonesha licha ya kukumbana na vikwazo vingi katika kazi yake.

“Kwenye Bongo Fleva nampenda sana Nay wa Mitego, I like that man(Ninamkubali sana), unajua binadamu ukisha kutandikwa, halafu ukasema to hell, ukarudi ukasema wapo, ni big respect (Heshima kubwa sana), kama unanisikiliza Nay, Ilove you”, amesema Fatma Karume.

Fatma Karume ameendelea kwa kusema kwamba msanii huyo ameonesha ujasiri mkubwa kwa kuendelea kufanya muziki, licha ya kufungiwa mara kadhaa, kitendo ambacho amekitaja kama uonevu.

Msanii huyo anatamba na wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina la ‘Alisema’ ambao ameuachia wiki hii na kuzua mijadala kutokana na maneno aliyoyatumia. 


TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker