News

Harry Kane yuko Fiti Kuivaa Liverpool

Mshambuliaji tegemezi na nahodha wa klabu ya Tottenham Harry Kane amesema yupo tayari kuvaana na Liverpool kwenye fainali ya Klabu Bingwa Ulaya Jumapili ijayo.

Harry Kane yuko Fiti Kuivaa Liverpool

Kane, 25, alipata majeraha makubwa ya kifundo cha mguu baada ya kuteleza na kuanguka kwenye mchezo wa robo fainali ya kombe hilo dhidi ya Man City Aprili 9.

Kocha wa Spurs Mauricio Pochettino awali alisema nahodha huyo wa Uingereza angelikuwa nje ya uwanjwa kwa mechi zote zilizosalia.

“Najisia vyema sana sasa. Sina shida tena,” amesema Kane.

“Nilianza kurudi kwenye kikosi toka mwishoni mwa wiki iliyopita. Wiki hii narejesha nguvu na ukakamavu wa mwili kwa kadri ya uwezo wangu,” amesema.

“Baada ya hapo itakuwa juu ya kocha kuamua. Yeye ndiye atafanya tathmini yake na kufanya maamuzi ya kunujumisha kikosini ama la. Lakini mpaka sasa mimi majisikia vizuri na nipo tayari kwa mchezo.

Kane ameifungia Tottenham magoli 24 msimu huu kwenye michuano yote licha ya kuwa nje ya uwanja kwa wiki sita baina ya Januari na Februari baada ya kuumia kifundo cha mguu huo huo alioumia mwezi uliopita.

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker