News

Kikosi cha Simba kilichopaa nchini Zambia

Kikosi cha Simba kimesafiri leo alfajiri kuwafuata Nkana Red Devils ya nchini Zambia tayari kwa mchezo wa kwanza wa hatua ya pili ya Klabu Bingwa Afrika wikiendi hii.

Kikosi cha Simba kilichopaa nchini Zambia

Kikosi hicho kimeongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Francis Ndulane pamoja na wachezaji 20, watu sita kutoka benchi la ufundi wakiongozwa na Kocha Mkuu, Patrick Aussems na viongozi watatu wa klabu.

Kikosi cha Simba kilichopaa kuelekea nchini Zambia ni:

Makipa: Aishi Manula, Deo Munishi Dida.

Mabeki: Nicholas Gyan, Mohamed Hussein, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Juuko Murshid.

Viungo: Jonas Mkude, James Kotei, Hassan Dilunga, Clatous Chama, Said Ndemla, Mzamiru Yassin, Haruna Niyonzima, Rashid Juma, Shiza Kichuya.

Washambuliaji: John Bocco, Emmanuel Okwi, Adam Salamba, Meddie Kagere.

Kikosi cha Simba kilichopaa nchini Zambia

Baada ya mchezo huo ambao utapigwa Jumamosi, Simba itarejea nchini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudio. Endapo Simba itavuka hatua hii ya pili, itafuzu hadi hatua ya makundi ya michuano hiyo, ambapo itakuwa ni historia kubwa kwa klabu hiyo baada ya miaka mingi kupita.

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker