News

Taarifa Mpya kumhusu Kocha Mkuu wa Simba SC

Kocha Mkuu wa Simba SC, Mbelgiji, Patrick Aussems, ameuambia uongozi wa timu hiyo kuwa, anataka kuendelea kukaa hotelini kwa kuwa amezoea na pia hajui kupika.Kocha Mkuu wa Simba SCAussems jana jumamosi aliiongoza timu hiyo kucheza dhidi ya Ndanda katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ukiwa ni wa tatu kwake na wa kwanza wa ugenini katika ligi ya msimu huu mechi ambayo timu yake hiyo ilitoka sare ya bila kufungana.

Ikumbukwe, Mbelgiji huyo alifikia katika Hoteli ya Golden Tulip ya Masaki kabla ya kuhamishiwa katika Hoteli ya Sea Scape iliyopo Mbezi Beach mara baada ya kuanza kazi kwenye timu hiyo na japo hulipa chumba Sh 170,000 kwa siku.

Aussems alisema hawezi kukubali kuishi kwenye nyumba za kupangiwa kwa kuwa maisha yake ya ukocha amekuwa akiishi hotelini.“Kwa hapa ndiyo sehemu ambayo nitaendelea kuishi kwa muda wote, nilishawaambia viongozi na hilo wanalijua hivyo siwezi kwenda kuishi kwenye nyumba yoyote zaidi ya hapa”.

“Unajua kwanza sijui kupika halafu maisha ya hotelini nimeyazoea tangu nimeanza kufanya kazi Afrika nimekuwa nikiishi hoteli sawa na hapa na uzuri huwa sichagui chakula ili mradi kiwe kitamu,” alisema Aussems.

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker