Kimataifa

Mahakama Kuu Rwanda yamuachilia Diane Rwigara

Mahakama Kuu mjini Kigali imeamua kumuachilia kwa dhamana mwanasiasa wa upinzani Diane Rwigara na mamake na watafuatiliwa wakiwa nje ya gereza.Mahakama Kuu Rwanda yamuachilia Diane Rwigara
Jaji wa mahakama kuu mjini Kigali ametangaza kwamba maombi yao ya dhamana yamekubaliwa lakini wakawekewa masharti ya kukabidhi Pasport zao kwa mwendesha mashtaka. Aidha wametakiwa kutovuka mipaka ya jiji la Kigali bila kibali maalumu.
Wawili hao walikuwa kizuizini tangu mwaka jana kwa tuhuma za kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka. Walikanusha madai hayo wakisema yana misingi ya kisiasa.
Mashtaka yanayomkabili Rwigara na mtetezi maarufu wa haki za wanawake nchini Rwanda na familia yake inasema matatizo yake yalianza wakati aliamua kuwania urais.

 

 

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker