News

Majaliwa Aipongeza Benki ya NMB

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa  Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo (wapili kulia) kuhusu kompyuta na madaftari kwa ajili ya shule wilayani Ruangwa pamoja na madirisha ya aluminium na milango kwa ajili zahanati ya Nandagala . Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Zahanati ya Nandagala Julai 28, 2019

Majaliwa Aipa Heko NMB

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Taasisis ya Jamii Bora, Yassir Salim wakati alipowasili kwenye Zahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa kupokea msaada wa vifaa vya hospitali vye thamani ya  ya shilingi milioni 250 vilivyotolewa na Taasisi hiyo ikishirikiana na Taasisi ya Helping Hand. Pia alipokea madirisha ya aluminiam na milango kwa ajili ya zahanati hiyo pamoja na kompyuta na madaftari kwa ajili ya shule wilayani  humo vyenye tahamani ya shilingi milioni 25 vilivyotolewa na Benki ya NMB. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya zahanati ya Nandagala Julai 28, 2019. Kulia ni Vicky Bishubo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali katika Benki ya NMB.

Majaliwa Aipa Heko NMB

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB baada ya kupokea madirisha ya aluminium na milango kwa ajili ya zahahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa pia kompyuta na  madftari kwa ajili ya shule za wilaya hiyo vyanye thamani ya sh.milioni 25 vilivyotolewa na NMB. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya zahanati ya Nandagala,Julai 28, 2019. 

Na. Mwandishi Wetu, Ruangwa
Bank ya NMB imekabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi, kompyuta, na Madaftari vyenye thamani ya Tsh. Milioni 25 kwa ajili ya kukuza sekta ya elimu na afya katika halmashauri ya Ruangwa Mkoani Lindi.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa leo July 28, 2019 kwa Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa ambae pia ni Mbunge wa jimbo hilo katika Zahanati ya Nandagala iliyopo katika Kijiji cha Nandagala Wilayani humo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali Bi, Vicky Bishubo alisema Vifaa hivyo vilivyotolewa ni pamoja na Madilisha ya Aluminiam kwa ajili ya Zahanati ya Nandagala yenye thamani ya Tsh. milioni 15, mabati 56 zikiwa na Mbao zake za kupaulia vyenye thamani ya Tsh. Milioni 3.3, Kompyuta 10 kwa ajili ya Shule ya Sekondari Kasimu Majaliwa pamoja na Madaftali yenye thamani ya Tsh. Milioni 5 kwa ajili ya Shule mbali mbali katika Wilaya hiyo ya Ruangwa.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa, Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali Bi, Vicky Bishubo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bank hiyo alisema kuwa kwa NMB changamoto za sekta ya Afya na Elimu hapa Tanzania ni jambo la kipaumbele kutokana na umuhimu wa sekta hizo kuwa ndio nguzo kuu ya maendeleo kwa Taifa.

“Sisi kama NMB tumekuwa msitari wa mbele kuchangia huduma za kijamii kwa lengo la kurejesha sehemu ya faida yetu kwa jamii, ambapo kwa zaidi ya miaka saba mfululizo tumeweza kuchangia 1% ya faida yetu kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii inayotuzunguka” alisema Bishubo

Hata hivyo Bishubo aliongeza kuwa kwa mwaka 2019 Benk yao imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 1 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo kusaidia sekta ya Elimu na Afya ambapo mpaka sasa tayari imeshatoa msaada wa zaidi ya Tsh. Milioni 600.

Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa aliishukuru Bank ya NMB kwa kutoa msaada huo ikiwa ni moja ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano

Majaliwa alisema kama Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Bank hivyo katika shughuli mbali mbali za maendeleo pamoja na majanga yanapotokea.

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker