News

Matola hajui hatima yake ndani ya LIPULI (+Video)

Na. Ahmad Abdallah, Lindi.

Baada ya kufanikiwa kuibakisha kwenye ligi kuu na kuifikisha kwenye hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam, timu ya Lipuli. Kocha mkuu wa timu hiyo, Seleman Matola amesema hajui hatima yake ndani ya timu hiyo.

Matola hajui hatima yake ndani ya LIPULI

Akizungumza na Lindi Yetu TV baada ya kumalizika mchezo wa fainali ya kombe la shiriko la Azam uliochezwa baina ya Lipuli na Azam, alisema hatima yake kuhusu kuendelea au kutoendelea kufundisha timu hiyo ipo mikononi mwa viongozi wa Lipuli.

Alisema kwasasa baada ya kumalizika ligi kuu na kombe la Azam anakwenda kukabidhi timu kwa viongozi ambao watajua hatima yake yeye ndani klabu hiyo.

‘Unajua kwa timu zetu hizi baada ya kumalizika mashindano wachezaji na dawati la ufundi mnakuwa huru,,‘ alisema Matola.

Aidha Matola amelalamika kubana kwa ratiba, hali ambayo imechangia timu yake kufungwa bao moja na Azam. Alisema aliwahi kulalamikia ratiba hiyo, matokeo yake wamejikuta wanatembea siku mbili barabarani kuja Lindi wakibakiwa na siku mbili kabla ya mchezo wa leo.

Licha ya kukubali matokeo ya mchezo huo, lakini Matola hakusita kusema uchovu wa wachezaji umechangia wapoteze mchezo huo.

Mchezo wa fainali wa kombe la shirikisho la Azam umechezwa leo katika uwanja wa Ilulu uliopo katika manispaa ya Lindi. Ambopo mgeni rasmi katika fainali hiyo alikuwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Tanzania, Kassim Majaliwa(MB).

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker