Wasanii

Melanin World Tour ya bendi ya Sauti Sol yaja Dar es Salaam!

Bendi maarufu kutoka Kenya, Sauti Sol, linawaletea onyesho la kipekee tarehe 15 Disemba 2018 pale Buckets, Masaki.

Melanin World Tour ya bendi ya Sauti Sol

Kabla ya kufika Dar es Salaam, Melanin Tour imewapa Sauti Sol fursa ya kucheza mziki wao kimataifa – kutoka Melbourne, Australia hadi Paris, Ufaransa. Na sasa, Dar es Salaam!

Sauti Sol inawaletea mziki wa kiroho, kutumia sauti zao na vyombo vya muziki (LIVE), ili kuwapa mashabiki tamasha pekee la mwaka.

Mwaka huu ulikuwa mwaka muhimu wa Sauti Sol. Walitoa midundo yao Short N’ Sweetna Tujiangalie, na nyimbo yaoMelanin ulipata mafanikio ya kimataifa barani Afrika. Wamecheza kwenye matamasha mbali mbali pamoja na wasanii wakubwa kama Major Lazor.  

Mwaka huu pia waliadhimisha miaka 10 tangu kutolewa albamu yao ya kwanza, “Mwanzo”. Tangu enzi za nyimbo za Lazizi”, Mama Papa na Blue Uniform, waTanzania wameendelea kuwa washabiki wakuu wa Sauti Sol. Bendi hili liko tayari kuonyesha tena Dar es Salaam na kurudisha upendo waliopata kutoka washabiki wa Tanzania.

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker