Wasanii

Mwana FA atoa ONYO kwa Wasanii wakiukaji wa Sheria

Msanii wa Bongo Fleva, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ amesema kuwepo kwake kwenye bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), haimaanishi wasanii wavunje sheria katika kazi zao.Mwana FA atoa ONYOMwanaFA ameyasema hayo leo Novemba 14, ikiwa ni siku moja tangu wasanii Rayvanny, Diamond Platnumz na lebo ya Wasafi kutozwa fainai ya Sh3 milioni kila mmoja kutokana na wimbo wa Mwanza ambao ulifungiwa ukidaiwa tungo zake kwenda kinyume na maadili.

Akizungumzia sakata hilo amesema hana maoni katika hilo na kukumbusha kwamba kuwa kwake Basata isiwe ndio sababu ya wasanii kuvunja sheria.

Alipoulizwa kama amepitia mashairi ya wimbo huo na kuona kama ni sahihi kufungiwa amesema kwa sasa hana cha kusema na kutaka apewe muda zaidi mpaka hapo atakapotoka kwenye kikao ambacho hata hivyo hakijajulikana kitaisha saa ngapi.

MwanaFA alifika katika ofisi hizo za Basata saa 6:00 na kuingia ofisi za Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Godfrey Mngereza na kueleza kuwa amefika kwa ajili ya vikao vyao vya kawaida japo hajui kama ya kina Rayvanny itakuwa moja ya mada watakayozungumzia.

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker