News

Namungo FC Uso kwa Uso na Lindi United Kesho Ilulu

Timu ya Namungo FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza yenye maskani yake wilayani Ruangwa kesho itakaribishwa na Timu ya Lindi United katika mchezo wa kirafiki ambao utachezwa katika Uwanja wa Ilulu.Namungo FcLindi United ni timu mpya ambayo imeundwa hivi karibuni na Siku ya kesho itakuwa ni mechi yake ya kwanza ya kujipima nguvu dhidi ya Namungo FC.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza majira ya saa 10:00 jioni na Kiingilio cha mchezo huo ni Tsh 1000/=.

Akizungumza na Lindiyetu.co.tz Mwenyekiti wa Muda wa timu ya Lindi United Hamisi Kirefu amesema kuwa Timu ya Lindi United inatarajia kushiriki mashindano ya FA kwa mwaka huu hivyo kwa mechi hii itakuwa na faida kwa kwani watajua kipimo cha timu yao iko katika hali gani.

Pia amewaomba wapenzi na mashabiki wa Mpira wa Miguu wa Mkoa wa Lindi na viunga vyake kujitokeza kwa wingi kesho Uwanja wa Ilulu kuiunga mkono timu yao ya Lindi United.

Timu ya Namungo Leo ilikuwa na Mchezo wa Kirafiki katika wilaya ya Kilwa ikicheza na timu ya Leicester na kufanikiwa kupata ushindi wa goli 3-0.

Magoli ya Namungo yalifungwa na Abeid Athumani kwa mkwaju wa Penati mnamo dakika ya 18 huku goli la pili likifungwa na Lucas Kikoti katika dakika ya 78 na lile la tatu likiwekwa kimian na Rajabu Mlangali mnamo dakika ya 85.

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker