News

Rais Magufuli awapa neno Wafanyabishara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewaonya wafanyabiashara wanaopandisha bei za vyakula katika msimu huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Rais Magufuli awapa neno Wafanyabishara
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya waumini wa Kiislamu na wadau wengine wakati akihitimisha mashindano maalumuya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019

Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo wakati akihutubia maelfu ya Watanzania waliofika katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kushuhudia mashindano maalumu ya 20 ya kusoma Qur’aan tukufu barani Afrika, yanayoandaliwa na taasisi ya AL-hikma ya nchini Tanzania.

Magufuli amesema kuwa kitendo cha kupandisha bidhaa hizo hakimpendezi mwenyezi Mungu kwani mfanyabiashara hawezi kutajirika kwa kipindi cha mwezi mmoja, bali ni kujichumia dhambi.

Rais Magufuli awapa neno Wafanyabishara
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Bi. Sumayyah Juma Abdallah wa Tanzania baada ya kupata alama 98.66 na kuibuka mshindi wa tano wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalum ya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019

Natoa wito kwa wafanyabiashara kuacha kupandisha bei za bidhaa ambazo zinatumiwa na ndugu zetu Waislamu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan, mamlaka za serikali zifuatilie suala hili kwa karibu”, amesema Rais Magufuli.

Ameongeza kuwa, “kufunga katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan au Kwaresma bila ya kuyaishi maneno yaliyo kwenye vitabu vitakatifu ni kazi bure, sote kwa pamoja tuungane kuwasindikiza wenzetu kukamilisha mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan“.

Kilele cha mashindano hayo kimehitimshwa kwa kutangazwa washindi watano kati ya 20 ambao walishindana kutoka mataifa kadhaa barani Afrika. Mshindi wa kwanza ni Mohamed Diallo (23) wa Senegal ambaye amejishindia zawadi ya Sh. 20 milioni pamoja na tiketi ya kwenda kuhudhuria ibada ya Hijjah nchini Saudi Arabia.

Rais Magufuli awapa neno Wafanyabishara
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Bw. Mohamed El Moujabba Diallo wa Senegal baada ya kuzoa Alama 99.88 na kuibuka mshindi wa Kwanza wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalumuya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019

Mshindi wa pili ni Faruq Karibu Yakubu (21) kutoka Nigeria zawadi yake ni milioni 12, mshindi wa tatu ni kutoka Zanzibar Shamsuddin Hussein Ali (22) ambaye amepatiwa sh. milioni 7, namba nne ni kutoka Niger Idrissa Ousmane (21) amekabidhiwa shilingi milioni 5 na mshindi wa tano ni Sumayya Abdallah (12) kutoka Tanzania zawadi yake shilindi milioni 3 na Rais Magufuli amemuongezea milioni moja kutokana na kuwa mshiriki wa kike pekee.

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker