Wasanii

RC Awataka Wasafi Waongeze Ushirikiano

WASANII wa Zanzibar na Tanzania bara wametakiwa kuimarisha mahusiano na ushirikiano baina yao ili kusaidia maendeleo ya muziki wa kizazi kipya katika pande zote mbili za Jamhuri ya muungano Tanzania.

RC Awataka Wasafi Waongeze Ushirikiano

Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa mjini magharibi alipokutana na timu ya wasanii kutoka lebo ya ‘Wasafi Clasic’ ya Dar es salam na Zenji Flavour Unity (ZFU) ofisini kwake Vuga walipomtembelea kuelekea tamasha la Wasafi Festival 2018 linalotarajiwa kufanyika Leo Usiku.

Ameeleza kuwa pamoja na kuwepo kwa mashirikiano ya muda mrefu, ipo haja pande mbili hizo kukaa chini na kufanya kazi pamoja ili kuimarisha vipaji vyao sambamba na kuwasaidia wengine kufikia malengo yao.

Ayoub ambae pia ni mlezi wa chama cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya Zanzibar alishauri kuanzishwa kwa mashindano ya kutafuta wasanii bora wa Zanzibar watakaoweza kuunganishwa na lebo ya muziki ya WCB rai ambayo iliungwa mkono na Afisa Mtendaji Mkuu wa lebo hiyo msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’ na mlezi wa lebo hiyo Said Khamis Fela ‘Mkubwa Fela.

Aidha Ayoub aliupongeza uongozi wa lebo hiyo na Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF kwa kukubali kuwajumuisha wasanii wa Zanzibar katika tamasha hilo jambo alilosema litawasaidia kujitangaza na kuongeza uzoefu wa kushiriki matamasha makubwa kama hilo sambamba na kuwataka wazingatie sheria na taratibu zinazosimamia sanaa nchini.

Nae msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’ amemshukuru Mkuu huyo wa mkoa kwa kuunga mkono kazi zinazofanywa na wasanii wa ndani na nje ya zanzibar jambo ambalo linawawezesha kuitikia kaulimbiu ya serikali zote mbili za kuwataka vijana kufanya kazi.

alisema, hatua ya serikali kuendelea kufuatilia shughuli zinazofanywa na wasanii zinathibitisha kuwaunga mkono ili wafikie ndoto zao jambo ambalo aliahidi kuliendeleza ili kundi kubwa zaidi linufaike.

Alieleza kuwa katika tamasha hilo mbali ya burudani wanayoitoa wameweza kufanya shughuli mbali mbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kutoa misaada katika taasisi za elimu, wajasiriamali na kwa Zanzibar wanategemea  kutoa misaada katika skuli na kituo cha afya cha Chumbuni ili viweze kutoa huduma nzuri kwa jamii.

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker