News

Utata wa milioni 300 kutafunwa, TFF Yafafanua

Shirikisho la soka nchini TFF, limejitokeza na kutoa ufafanuzi juu ya taarifa zinazosambaa kuwa ndani ya chombo hicho cha juu cha soka nchini, kuna ubadhilifu wa shilingi milioni 300.

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, TFF imeeleza kuwa tayari suala la mahesabu ya pesa hizo lipo chini ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ambao nao walilifikisha mahakamani.

”Suala hili lipo ngazi ya mahakama hivyo TFF inaona ni vyema iviachie vyombo vya kisheria vifanye kazi yake kwa mujibu wa taratibu”, imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa iliyosambaa inaelezea zaidi juu ya hesabu za shirikisho hilo kati ya mwaka 2015 na 2016 ambazo zilitolewa Septemba 11, 2016 na Novemba 27, 2017.

Utata wa hesabu hizo ulipelekea baadhi ya waliokuwa viongozi wa shirikisho hilo kwa wakati huo akiwemo Rais Jamal Malinzi kushikiliwa na kufunguliwa kesi ambayo bado inaendelea mpaka sasa.

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker