´╗┐
News

Wakazi wa Itilima Wafurahia Kukamilika Mradi wa Maji

Na Benny Mwaipaja,WFM, Simiyu

ZAIDI ya Wakazi elfu 2 wa Mjiwa Lagangabilili, Tarafa ya Kanadi, Wilayani Itilima, mkoani Simiyu, wameondokana na adha ya kukosa maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mradiwa maji ya bomba wa Lagangabilili uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 900.

Wakazi wa Itilima Wafurahia Kukamilika Mradi wa Maji

Wakizunguza mbele ya timu maalumu ya wataalam wanaofuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutoka baadhi ya Wizara wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, Baadhi ya wakazi waMji huo wa Lagangabilili wameishukuru Serikali kwa kuwapatia mradi huo wa maji.

“Tunaishukuru sana Serikali kwa kutuletea maji tunayapata kwa urahisi, zamani tulikuwa tukihangaika sana akina mama walikuwa wakiyafuata mto Simiyu, mbali sana, walikuwa wakitoka saa kumi usiku na kurudi saa tatu asubuhi” alisema Bw. Chonza Maduhu, mkazi wa Lagangabilili, Simiyu

Mhandisi wa Maji wa Wilayaya Itilima, Bw. Goodluck Masige, amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kumefanya kiwango cha upatikanaji maji safi na salama kwenye mji huo ambao ndio makao makuu ya wilaya ya Itilima, kupanda kutoka asilimia 20 za awali hadikufikia asilimia 100.

“Tumejenga tenki lenye ujazo wa lita 225,000, vituo 21 vya kuchotea maji, tumejenga mtandao wa bomba za kusambaza maji nyenye urefu wa mita 29,000 na kufunga pampu 1 ya kusukuma maji” aliongea Mhandisi Masige

Ameitaja kazi iliyosalia kukamilisha mradi huo unaotarajiwa kukabidhiwa Serikalini na mkandarasi, Kampuni ya M/S Nangai Contractors and Engineering Co. Ltd, Disemba 30, 2018, kuwa ni ujenzi wa birika la  kunyweshea mifugo(Cattle trough).

Mmoja wa Wajumbe wa timuya Kitaifa ya ufuatiliaji wa miradi ya maji katika mikoa ya Simiyu na Mara, Bw.Jordan Matonya, amesema kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha kuwa miradi inayotekelezwa maeneo mbalimbali nchini inatekelezwa kwa viwango vya hali yajuu na kuwanufaisha wananchi.

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker