News

Watu Wafurika Nyumbani Kwa MO Dewji (Video+)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekanusha taarifa zinazodai kuwa Mohammed Dewji ‘Mo’ amepatikana lakini nyumbani kwa mfanyabiashara huyo watu mbalimbali wamekuwa wakiwasili.Watu Wafurika Nyumbani Kwa MO DewjiMwananchi limefika nyumbani kwa Mo maeneo ya Oysterbay jijini Dar es Salaam na kushuhudia ndugu, jamaa na marafiki wakiingia nyumbani kwa mfanyabiashara huyo.

Nje ya nyumba hiyo kuna ulinzi mkali wa kampuni binafsi, lakini magari ya ndugu na jamaa na marafiki yamekuwa yakifika mfululizo.

Baadhi ya ndugu hao wakigoma kurekodiwa wamesema ndani kwa Mo hakuna taarifa sahihi kama amepatikana na kilichopo ni bado ndugu yao hajulikani aliko. Baadhi ya ndugu wa kike wamekuwa wakiingia huku wakilia.

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekanusha taarifa za kupatikana kwa mfanyabiashara huyo aliyewahi kuwa mbunge wa Singida Mjini (CCM).

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker