News

Waziri ajibu kuhusu matukio ya utesaji wapinzani

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Agustino Mahiga, amesema matukio ya utesaji ya wapinzani na uvunjifu wa amani pamoja na madai ya wapinzani ni miongoni mwa mambo yanayoulizwa na Jumuiya za Kimataifa na serikali inaendelea kuyafuatilia.

Waziri ajibu kuhusu matukio ya utesaji wapinzani

Waziri Mahiga ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma katika muendelezo wa vikao vya Bunge baada ya kuulizwa swali na Mbunge wa CUF Ali Saleh, ambaye alihoji juu ya uwepo wa matukio hayo na kueleza ni uvunjaji wa haki za binadamu.

Akijibu swali Waziri Mahiga ameeleza kuwa “kuhusu matukio ya utesaji wa wapinzani na uvunjaji wa haki za binadamu, matukio yanajulikana serikalini na vyombo vya usalama vinafuatilia.”

Mara nyingi tunapata taarifa na majibu yanaridhisha, kazi ya upelelezi inaweza kuchukua muda, maswali haya yanaulizwa na wananchi, yanaulizwa kimataifa, tupo tayari kutoa taarifa sahihi uchunguzi ukikamilika” ameongeza Mahiga

Kwa sasa Bunge linaendelea jijini Dodoma, ambapo Mawaziri mbalimbali wameendelea kuwasilisha makadirio yao ya bajeti na wakiomba ridhaa ya kupitishwa na wabunge.

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker