News

Yanga Yaendelea Kujitanua Kileleni ligi Kuu

AZAM FC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam jana jioni.

Yanga Yaendelea Kujitanua Kileleni ligi Kuu

Matokeo hayo yanaiongezea pointi moja Azam FC na kufikisha 40 katika mechi ya 16, sasa wakizidiwa pointi moja tu na vinara, Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi 15.

KMC ilitangulia kwa bao la George Sangija dakika ya 18 kabla ya Azam FC kusawazisha kiungo Mzimbabwe, Tafadzwa Kutinyu dakika ya 45.

KMC tena wakaitangulia Azam FC kwa bao la Rayman Mgungila dakika ya 63, kabla ya mshambuliaji Mzimbabwe Donald Ngoma kuisawazishia timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake dakika ya 85.

Mchezo mwingine wa Ligi Kuu uliochezwa hapo jana, Lipuli FC imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Mabao ya Lipuli ya kocha Suleiman Matola yalifungwa na Miraj Athumani ‘Madenge’ dakika za 36 na 43, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na Said Dilunga dakika ya 90 na ushei.

Kufuatia ushindi huo, Lipuli FC inafikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi 16 na kupanda kutoka nafasi ya 15 hadi ya 10 kwenye msimamo wa ligi, wakati Ruvu inayobaki na pointi zake 17 za mechi 16, inaporomoka kwa nafasi moja hadi ya 15.

YANGA YAENDELEA KUJITANUA KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAPANA)
Tags
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker